Friday, July 5, 2019
ISHARA ZA MWANAMKE ANAYEKUZIMIA
1. Mnapokutana na kuongea
Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea, ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu. Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia. Sikiliza sauti yake, kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini. anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.
2. Ajali za kijitakia
Anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike. Anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia, au anakukumbatia.
3. Anaibia kukuchunguza
Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko bize na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.
4. Anapenda mgusane
Mwanamke anayevutiwa na wewe mnapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako, au unapokutana naye anaweza kukukumbatia.
5. Anatafuta ukaribu
Mwanamke aliyevutiwa na wewe anapenda kuwa karibu na wewe muda wote. Mfano akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta, ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe. Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga, hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe.
6. Anapenda umjali
Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.
7. Hawezi kuzuia tabasamu
Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee, hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.
8. Ishara za mwili
Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini. Kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamwona anashtuka gafla.
9. Anafurahishwa na vituko vyako
Mwanamke anayekupenda daima ni mwenye furaha mkiwa pamoja. Huwezi ukamboa, hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.
10. Anakujali
Anakuwa anakujali, mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza “unahitaji chochote? unaweza ukasema “nina kiu ngoja ninunue maji” utamsikia “nina maji, kunywa haya yangu kwanza”.basi ujue kwamba anakujali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment