Monday, July 1, 2019

SIFA ZA WIFE MATERIAL


Mtu yeyote anapenda kuwa wa thamani, mtu au kitu kuwa wa thamani inategemea sana matumizi yake na tabia yake, hasa tabia. Tabia ya kitu au mtu ndio hupelekea ubora wake kubaki kama ulivyo au kupungua. Hali na mazingira yanapobadilika kitu bora hubaki kama kilivyo na thanmani yake kuzidi kuongezeka. Chumvi ikichanganywa na mchanga utatafuta mbinu ya kuitoka kwenye mchanga ili uitumie, na ukiamua kwenda kuiuza chumvi hivyo iliyotolewa kwenye mchanga gharama yake haitakuwa ile ya mwanzo.
Inaweza kuleta shida kidogo kujadili thamani ya mwanamke pekee wakati huo huo wote wawili mwanamke na mwanaume wanathamani sawa. Nafahamu kuwa wanaume wenzangu wanathamani sawa na mwanamke lakini ukiangalia leo duniani mwanamke huenda hajithamini au athaminiwi jamii yake.
Chanzo kikubwa ni mwanamke yeye mwenyewe na ufahamu wake uliojaa mtazamo wa kusaidiwa na kutaka kuthaminiwa pasipo sababu ya msingi. Kamwe mwanamke hata thaminiwa asipo baki kwenye ubora wake. Thamani iliyo ndani ya mwanamke ni kubwa sana kuliko mwanaume, lakini itakuchukua muda kuonesha ukubwa wake.
Tabia nyingi za kumfanya mwanamke wa kisasa awe wa thamani ni zile zinazoonekana zimepitwa na wakati. Jaribu kufanyia kazi hizi tabia, moja hadi nyingine kila siku na utaona faida ya kuwa mwanamke.
Moyo wa shukurani
Mwanamke hayupo juu ya kumshukuru mtu yeyote, bila kujali ni mtu wa aina gani au umri wake. Huonesha hali yake ya kushukuru bila ya wasiwasi.
Ni kiongozi
Waanawake wanaushawishi mkubwa sana kwa jamii. Licha ya kwamba wengi wao hawafahamu hivyo ndio maana wanalilia kuwezeshwa. Mwanamke anaweza kuwa kiongozi mkubwa na mfanya maamuzi kupitia nguvu ya ushawishi kwa watenda kazi wengine wanao mzunguka.
Mwanamke mvumilivu
Sifa kubwa ya mwanamama yeyote ni uvumilivu. Hayumbishwi na hali yeyote, mtu wa malengo na uhakika wa kufanya kitu. Haruhusu msukumo wowote kumrudisha nyuma au kumwangusha.
Anayetetea maadili ya jamii
Mwanamke amepewa majukumu ya asili ya ulezi wa jamii kutokana na kazi nzito aliyonayo ya kuzaa. Anachukua muda kutafuta tatizo na kulitatua kabla jamii haijaharibika.

Mwaminifu
Mwanamama anayetunza makubaliano na ahadi kama kitu cha thamani huyo anafaa sana jamii. Asiye mgomvi wala kujibizana ovyo na mwanaume.
Anayejitambua
Anayefahamu nini cha kufanya na ni mwepesi wa kutambua makosa yake na kuomba msamaha bila shuruti. Kifua aliumbiwa mwanaume ili akitanue na apate kigugumizi kusema samahani. Lakini kwa mwanamke samahani ni kitu chepesi sana.
Anafikiri kabla ya kusema
Jamii inamtazama mwanamke kwa jicho la kungojelezea, anachotamka midomoni mwake kinapokelewa na akili za wengi aliowahi kuwalea ama kuwazaa. Midomo yake kama inavyopambwa hivyo na maneno yake yawe ili kujenga na si kubomoa.
Ni mtu wa ubora wake wa kipekee
Huyu mwanamama hatumii uzuri wake na akili zake kupata kujulikana na kukubaliwa na watu wengine. Bali huweka hazina hiyo kwa kuenenda katika ubora wake wa pekee na kushawishi wengine kufuata mfano.
Mtu anayependa kuwatunuku wengine.
Hutoa kipaumbele kwa wengine kupitia vitu vichache alivyo navyo, kama kawaida ya mwanamke kulea jamii inayomzunguka.
Midomo yake haina umbea.
Maneno ya umbea huonesha moyo wako umejawa na nini. Mtu wa namna hii hafai kufanya lolote kati ya hayo uliyosoma juu.
Hujiwasilisha vizuri kwenye mitandao ya kijamii
Mwanadada ya kisasa anamtihani mmoja unaofananishwa na mtihani wa hisabati nao ni matumizi ya mitandao ya kijamii. Ngono na uchafu ndio vilivyojaa kwenye ukurasa wa mwanadada wa Kiswahili akihisi ndio ustadi wa matumizi ya mitandao. Unachotuma kwenye mtandao wa kijamii kila siku ndio wastani ya mawazo yako kwa siku husika.
Mkarimu
Hata kama hana sifa ya ukarimu atajitahidi kuwa mkarimu japo kwa muda. Mwanamke anafanya kila linalowezekana ili wageni wake waliomtembelea wawe na amani na huru. Hii hata kwa jamii ya watu masikini yhuko tayari kutengeneza utu wa muda hata kama anaroho mbaya ili tu awakarimu watu.
Mwenye kujizuia
Akiwa mkorofi lakini anaweza kujizuia pale anapokutana na mwanaume. Anaweza kuwa kutengeneza mazingira ya ili asiwaudhi walimzunguka, akaficha tabia yake mbaya kwa muda. Sio jambo zuri sana, ila angalau awe anaweza kufanya hivyo, siku akishindwa anakuwa moto wa kuotea mbali.
Ana mipaka kuhusu maisha yake.
Kuwa mkarimu haimaanishi kuwa unafanya kila unachoambiwa ufanye. Mwanamama shupavu huchora mipaka ya maisha yake katika jamii, maisha kama mahusiano, ndoa na mengine mengi ambayo ni hatari kuyafanya yawe ya jamii nzima.
Huonesha kupendezewa na wengine
Mwanamke hupendelea pia, sio yeye kupendelewa tu.
Mwenye heshima
Mara zote mwanamke hutoa heshima pale inapotakiwa kutolewa bila ya kujali itikadi yeyote. Hii ni pamoja na kukubali kitu alichofanya mwengine bila ya kinyongo.
Ni halisi
Ana watu anawahusudu lakini haigi kile wanachofanya na kufanya maisha yake yakawa batili. Hajifananishi na mtu yeyote na anaamini kuwa kuhamasishwa na Mungu ndio njia pekee ya kufanikiwa kwake.
Anajua ni wakati gani wa kuacha mambo yaende
Huinua siraha yake na kupambana kwa vile anavyovipenda maisha huku akijua kukwazwa na kuvunjiaka moyo kupo. Mambo hayo huumpa nguvu ya kusonga mbele, na anabaki mwenye matumaini Mema.
Mnyeyekevu
Anaruhusu wengine wainuke na kushamiri bila ya kinyongo.
Rahisi kubadilika
Mwanamama anaweza kuendana na mazingira yeyote na kuwa na kujiamini kama kawaida yake.
Ana huruma
Yupo tayari kumlinda na kumfadhiri yeyote anayehisi kuwa ni mpweke.
Anajivunia mwonekano wake.
Mungu amewajalia wanawake wengi wana mwonekano mzuri na huenda wanajua hilo. Hii wengi wanafanya, kujivunia walivyo licha wa wachache wanaotaka kuwa kama wengine.
Hujali afya na usafi wake
Anafahamu kuwa hawezi kufanikiwa kama hata jatajali afya yake kwanza. Anaweza kubeba mkoba mkubwa umejaa vitambaa vya kujifutia jasho, midomo, miguu na kusahau nauli ya kulipia usafiri.
Mara zote hujifunza na anafundishika
Sio mtu mjuaji wa vitu vyote anavyo kutana navyo. Hutoa fursa kwa watu wengine wamfundishe.

Msikilizaji mzuri
Hupenda kusikiliza anayoambiwa sio kila kitu anachoambiwa anajifanya anajua. Hasemi, “huniambii kitu kipya”, “nilishapitia hayo”, “nilijua tu”.

Mleta amani
Hachangii magomvi baina ya marafiki, aanzishi fitna mtaani kwao au eneo la kazi kupelekea kuvunja amani. Sio mwiba kwa wengine.
Mwadilifu
Mwanamke anafanya mambo mazuri hata pasipo tarajiwa kufanya. Mfano anabariki watu wanaomnenea mabaya.
Anasimamia ukweli
Anasimama na ukweli hata kama haukubaliki na watu wengi kwenye eneo analoishi. Hafati mkumbo.
Ana moyo wa haki
Mwanamama jasiri ana uwezo mkubwa wa kujua jema na baya. Na ana hisia juu ya kumwona mtu aliyeonewa anapata ukombozi.
Imani yake ni kwa Mungu
Mwanamke anajua kuwa utambulisho wake unatokana na aliyemuumba. Nguvu zake na maono yake yanatokana na maombi ya kila siku.
“kuwa msichana ni kwasababu ya kuzaliwa, kuwa mwanamke ni kwasababu ya umri bali kuwa wa thamani ni maamuzi”

No comments:

Post a Comment