Saturday, July 6, 2019

JINSI YA KUMPATA UMPENDAE NDANI YA DAKIKA CHACHE


Mara nyingi wengi wa wadada na wakaka wameshindwa kujua au kusoma ishara za pale wanapovutiwa au wanapokuwa wamevutiwa na mtu ambaye kwa Mara ya kwanza wanaweza kujuana na kuwa wapenzi au marafiki.

Hebu fikiria imetokea Mara ngapi kwa baadhi ya wadada au wakaka wakakutana siku ya kwanza na kisha wakaunda mapenzi na wengine hufikia kufanya mapenzi kabisa katika siku ya kwanza tu wanapokutana.
Unadhani ni uchawi?!
Unadhani ni maajabu?!
Usiwaze sana,, Ni jambo la kawaida sana hasa ukijua baadhi ya ishara na kujua kusoma lugha ya matendo ambayo kwa mdada au mkaka mliyeonana nae kwa Mara ya kwanza atakayokuonesha na kisha ukaweza kuongea nae kwa Mara ya kwanza pasipo kutumia maneno. Lugha ya macho au lugha ya matendo ina nafasi kubwa sana katika mahusiano pengine kuliko maneno ya kawaida.
Leo katika post hii nitapenda kuzungumzia suala moja tu la Lugha ya macho na jinsi inavyoweza kumshawishi mwenzio hadi mkaanza kujenga urafiki.
Lugha ya macho ina nafasi kubwa sana hasa pale mnapokutana pengine kuliko maneno yenyewe. Wanasaikolojia wanasema Lugha ya macho ina zaidi ya 70% katika kushawishi na kumfanya mtu aanze kukupenda.
Msichana huanza kuvutiwa na mwanaume ndani ya sekunde kadhaa baada ya kumuona mvulana. Hii humfanya mdada amuangalie mvulana kwa sekunde kadhaa. Ila hapa niweke jambo moja sawa, kwamba msichana huvutiwa na mvulana na humuangalia kwa matamanio ndani ya sekunde chache lakini pia hupoteza mvuto huo ndani ya muda mfupi endapo hakutaonekana jibu lolote kutoka kwa mwanaume. Ikumbukwe kuwa nilikwisha kueleza hapo mwanzo kuwa msichana huvutiwa zaidi na mvulana ndipo huanza kumuangalia, lakini pia ikumbukwe kuwa lugha ya macho huzungumza zaidi kuliko matendo na hapo msichana hutegemea zaidi lugha ya matendo imjibu vilevile kutoka kwa mvulana.
Msichana anapomuangalia mvulana humaanisha kuvutiwa hivyo mvulana hutakiwa kuonesha kwamba amemuona huyo msichana na kumuonesha kwamba anacho kitu pia kwa ajili ya huyo msichana. Mvulana huweza kutabasamu huku akimuangalia huyo binti na hapo huenda akawa ametoa jibu sahihi kwa msichana.
Kama ambavyo post zilizopita tuliona NGUVU YA TABASAMU KATIKA MAHUSIANO unaweza kurejea kujua tabasamu lina nguvu gani katika mahusiano .
Pia ieleweke kwamba msichana huonesha ishara ya kwanza na pia hupoteza mvuto endapo hataona jibu lolote kutoka kwa mvulana. Hivyo Mara umuonapo msichana anatabasamu huku anakuangalia jua dhumuni lake pia unapaswa kujua lugha anayozungumza na mtoto wa kiume unapaswa kujiongeza ili kumfanya azidi kuvutiwa zaidi na wewe.
Kwa Leo naomba kuishia hapo. Endelea kusoma zaidi APP Yetu kwa mambo mbalimbali yatakokupa vitu muhimu katika mahusiano na maisha ya mapenzi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment