Wednesday, July 10, 2019

SABABU AMBAZO HUCHOCHEA MWANAMKE AKUSALITI


Mapenzi ni matamu ukipata mpenzi mnaependana. Mahusiano mengi huvunjika na chanzo kikuu huwa ni ‘uplayer’ kama ninavyopenda kuuita namba sita mgongoni. Lakini wanaume wengi hujiuliza kwa nini mwanamke wangu hatosheki na mimi. Tatizo litakuwa ni wewe mwanaume ndie unayechangia ama pia labda ni mkewako ambaye ana shida. So leo hapa tumekuja na majibu kamili uzijue kwa nini wanawake wengi huplay wanaume zao.
#1 Tamaa.
Tamaa huvunja mahusiano mengi. Si kila mwanamke anapenda alivyo ilhali wengine wanaweza kuwa wanapenda pesa. Hivyo basi kama wewe ni mwanaume na mfuko wako hauna kitu basi ujue si kila mwanamke anaweza kuishi na wewe. Hivyo basi usitarajie uwe hauna kitu ukadhani kila mwanamke anaweza kuvumilia na hali ulionayo. Mwanamke hutafuta mwanaume atakayetimiza mahitaji yake na wewe uwe tu kama msaada wake.
#2 Mapenzi.
Je wewe uko bora kitandani. Swala hili mara nyingi husumbua sana. Kila mwanamke ana kiwango chake cha kufika kileleni. Mwanaume kama huwezi kumridhisha mkeo kitandani basi jua kuwa kunaweza kutokea matatizo. Wanawake wengine hutafuta wanaume ambao wanaweza kuwaridhisha kitandani na wewe ukawa mwanamke jina tu.
#3 Tabia.
Hapa napo kuna tatizo. Wewe mwanaume tabia zako ni zipi? Huezi tarajia uwe na tabia zinazokera na mimi niwe niko na wewe tu. Ok, sawa pesa unazo sikatai lakini je, mlo wako ukoje? Uvaaji wako ni upi? Mazungumzo yako ni ya aina gani? Tabia ulizo nazo kama ni mbaya hata siwezi kutoka na wewe mbele za watu. Haoa sasa itabidi nikatafute mwenzako ambaye naweza toka out nae.
#4 Distance.
Hii nayo pia huchangia sana wanawake kutokuwa waaminifu. Mapenzi yamenizidia na wewe uko mbali baba nifanyeje? Nitavumilia sawa lakini itafika pahali nitashindwa. Rafiki zangu kwa raha zao na wapenzi wao mimi huku navumilia nitashindwa. Pia hapa si kila mwanamke si mwaminifu. Kuna wengine ambao wanaweza kuvumilia pia. Hivyo basi yategemea na mtu mwenyewe. Lakini distance mara nyingi huvunja mahusiano.
#5 Mawasiliano.
Je wewe hutumia muda mwingi kuwasiliana na mpenzi wako? Waeza pata mwanaume anakaa mwezi mzima bila hata kumjulia hali mpenzi wake. Mawasiliano ni muhimu sana katika maisha ya wapenzi wawili. Ukikaa muda mrefu bila hata kutoa sababu ya kimya chako mwanamke anaweza kufikiria umemuacha.

No comments:

Post a Comment