Thursday, July 4, 2019
MAONGEZI 6 YA KUMFURAHISHA MPENZI WAKO
#1. Kufananisha.
Hii inaweza kukushangaza, lakini kama binadamu, hupenda kujifananisha na wengine kama tunataka kufurahia kuhusu sisi wenyewe. Yalinganishe mahusiano yenu ya mapezi na mahusiano ya kimapenzi ya marafiki zenu wa chuo au kazini.
Wote mtajisikia furaha kama mahusiano yenu ni mazuri zaidi ya wengine. Na kama kuna kitu mnakitamani kutoka kwenye uhusiano wa wenzenu, wote kwa pamoja mtajikuta mnafana mabadiliko ili kuimarisha maisha yenu ya kimapenzi.
#2. Ndoto za baadae.
Ongeleeni kuhusu matarajio yenu na ndoto zenu katika maisha. Maongezi ya aina hii huwafanya kuzijua ndoto za mwenzako na matarajio yake ya baadae na ni jinsi gani mnaweza kusaidiana ili kuyafikia malengo yenu. Hii inawafanya muwe karibu zaidi.
#3. Pendekeza.
Jitahidi kuwa mbunifu kidogo bhanaa. Au tunasema toa comment. Kama asubuhi aliondoka akiwa na nywele salu salu mwambie, lakini kama alipendeza mbwambie. Hii itawafanya wote mtabasamu.
#4. Vitu vipya vya kujaribu wakati ujao.
Usifikiri huu ni mda wa kuwaza mambo magumu katika maisha kama nlivyokuambia hapo awali. Badala yake kama kuna changamoto pendekeza njia sahihi inayoweza kulitatua hilo jambo, lakini mambo mapya katika uhusiano wenu kama kwenda honeymoon kwa ajili ya exposure na vitu vingine. Kuongelea mambo ambayo yanalenga kuboresha maisha yenu inafanya maongezi ya kitandani kuwa matamu sana.
#5. Likizo na Exposure.
Hakuna kinachofanya maongezi ya kitandani kuwa matamu kama kuongelea na kupanga sehemu za kutembelea baada ya miezi minne ijayo, kwa mapumziko na mpenzi wako au kwa lengo na kubadilisha mazingira na kujifunza(exposure). Jaribu kujadii ni sehemu gani nzuri za kwenda mambo ya kufanya, na mambo mengine mazuri mnayoweza kuyafanya wakati wa likizo. Hii itawafurahisha wote na itawasukuma kujituma zaidi katika maeneo yenu ya kazi na ndoto zenu zitatimia kwa uharaka zaidi.
#6. Kumbukumbu za kimahaba(Romantic Memories).
Kuongelea mapenzi yenu ni kitu kizuri kitandani. Muulize mwenzio kama anakumbuka siku ya kwanza alivyokukiss ilikuaje, kama alikua anaogopa mueleze, itamfanya akumbuke mbali na kutabasamu. Maongezi ya aina hii yataanzisha mada nyingine, hivyo hamtapungukiwa na mtajikuta mnajiona wa bahati nyie kuwa pamoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment