Thursday, June 27, 2019
BIKRA YA MWANAMKE NI NINI?
Bikira ni mwanamke au mwanaume ambaye hajawahi kufanya mapenzi (penetrative sex) na si lazima awe mwanamke ambaye atatoa damu siku ya kwanza ya tendo la ndoa.
Ni vizuri kufahamu kwamba asilimia 20% - 25% ya mabikira huwa hawatoi damu yoyote kutokana na muundo wa kizinda (hymen)
Wakati mwingine kizinda huondolewa kwa kufanya mazoezi mazito, kupanda baiskeli, kukwea miti na ifahamike kwamba kufanya mazoezi hakuwezi kuondoa ubikira.
Kizinda ni nini?
Kizinda ni ngozi nyembamba
sana (membrane) ambayo huziba entrance kwenye uke.
Ina matundu ambayo hutofautiana kwa size ambapo damu ya mwezi kwa mwanamke huweza kupita kila mwezi.
Kuna aina Nne za vizinda
1. Kizinda cha kawaida (normal hymen),
2. Kizinda kisicho na tundu lolote [huhitaji surgery wakati mwingine] (Imperforated hymen),
3. Kizinda chenye tundu dogo sana (Microperforated hymen)
4. Kizinda chenye tishu za ziada na kufanya matundu mawili (septate Hymen)
Bado haijajulikana kazi ya kizinda ni nini, kwani baada ya sex mara ya kwanza huchanika na kuachana na kubaki historia.
Kizinda kiligunduliwa mwaka 1544 na Daktari wa kiarabu Ibn Sinna hata hivyo kufika karne ya 16 watu walikuwa wana imani potofu kwamba kizinda ni ugonjwa na dawa yake ilikuwa ni sex inayofuatana na mwanamke kuolewa.
Kutokuwa na kizinda au kutokutoa damu siku ya kwanza ya sex si evidence kwamba mwanamke si bikira wapo wanazaliwa hawana wengine nyembamba sana na wengine huweza kutoka kutokana na aina ya mazoezi au accidentally.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment