Friday, June 28, 2019

KWANINI WANAUME HUWA WANACHEPUKA...!?


Leo nimeamua kuja na sababu zinazotokana na tafiti za wanaume kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano na ndoa. Ikumbukwe kwamba sababu za wanawake kutokuwa waaminifu hazifanani moja kwa moja na sababu za wanaume, na hata kitendo chakutokuwa mwaminifu kwenye ndoa kwa mume au mke pia huathiri ndoa husika katika uzito tofauti. Hii ni kutokana na sababu za kiasilia, kiuumbaji, kijinsia na kisaikolojia.
Zifuatazo ndizo sababu za wanaume wengi kuchepuka:
Kisasi.
Mara nyingi wanaume hutumia kitendo cha kutoka nje ya ndoa au nje ya mahusiano kama fimbo ya kulipiza kisasi kwa maumivu au hasira yoyote aliyokuwa nayo dhidi ya mpenzi au mke wake. Kwa mfano, wanaume wengi nilioongea nao binafsi, hususani wale ambao walikuwa wanalalamika kuwa mke wangu haniheshimu, mke wangu ananidharau, mke wangu hanisikilizi, mke wangu anafanya hivi au anafanya vile, wengi baada ya kuongea au kulalamika kwa muda mrefu pasipo kuona mabadiliko baadaye waliamua kuanza ku “cheat”.
Kisaikolojia, mwanaume anapochepuka kwa sababu ya kisasi, huwa inamwondolea ile hali ya kujishtaki au kushtakiwa nafsini kwamba amefanya kosa “guilty conscious” na hiyo inaweza kumfanya aendelee kuchepuka kwa muda mrefu tu, tofauti na mwanamke anapochepuka.
Ni vema ukachukua tahadhari hii, pale unapoona mume wako analalamika sana kuwa haumuheshimu, unamdharau, haumsikilizi, haushuki au kunyenyekea basi fahamu kwamba kunauwezekano mkubwa ameshaanza kuchepuka au yuko kwenye kuisoma ramani ili aanze. Kama kunauwezekano wa kubadili tabia

No comments:

Post a Comment