Friday, June 28, 2019

DALILI ZA MPENZI MWENYE MCHEPUKO


Ushawahi kuwa na hisia kuwa mpenzi wako labda ana mchepuko? Umekuwa ukijaribu kufanya utafiti wako wa kina lakini kila ukijaribu kupekua unaambulia patupu?
Ok. Leo kwa haraka tumekuja na ishara ambazo unaweza kuziangalia kwa mpenzi wako kama anachepuka au la.
Hapa Nesi Mapenzi tuko hapa kukujuza. Hivyo basi jukumu lako pia uhakikishe unawajuza marafiki zako. Ukiwa unashuku rafiki yako anamegewa basi usisite kumrushia na yeye chapisho hili pia yeye afunguke macho.
Well, mpenzi wako akiwa anachepuka basi inamaanisha jambo moja, wewe utakuwa ni number 2 automatic. Hivyo usikubali kamwe kuwekwa katika hali kama hii. Zama nami!
#1 Huwa anasumbuliwa na wasiwasi.

Ukitaka kujua kama mpenzi wako anachepuka, basi mwambie akupeleke zile sehemu ambazo anakuwa akitembea wikendi ama nyakati za jioni. Hapa utamwona kwanza akianza kutoa visababu visivyo eleweka. Na pindi akikubali kutoka na wewe basi hatakuwa makini na wewe bali atakuwa na wasiwasi asije akapatikana ghafla na mchepuko wake.
#2 Sikiliza moyo wako.

Ok, hii ni ishara ambayo iko ndani ya fikra zako. Ijapokuwa watu hawaamini kuwa fikra zako zinaweza kukupatia jawabu, ukweli ni kwamba kuna asilimia 100 kuwa unaweza kuwa kweli. Mfano umekuwa na huyu mwanamke kwa kipindi cha mwaka mzima. Halafu ukaona matendo yake yamebadilika ghafla. Unamwona anafalia nguo za kurembesha, anapaka marashi akiwa anatoka out na kadhalika. Hapa fikra zako zikikuambia kuwa anakucheat basi kunaweza kuwa na ukweli ndani yake.
#3 Hapatikani wikendi.
Hapa kila Siku za weekend anajifanya yupo bize au hapatikani au anaumwa ujue kabisa ameanza kukutoa moyoni kidogo dogo,Aina hii ya sababu huanza tararibu lakini baadae anaweza akakukatalia kabisa kua usiwe unasumbua weekend kwani anakua ana kazi kama kufua pia anaenda kanisani

No comments:

Post a Comment