Saturday, June 29, 2019
FAIDA ZA KUWA SINGLE KWA WAKATI FULANI
Katika sayari hii ya dunia kuna baadhi ya watu wanakwambia mapenzi ndiyo yanayoiendesha dunia, hii ni kwa sababu asilimia kubwa ya watu wengi wametawaliwa na mawazo ya kimapenzi.
Pamoja na kuwapo kwa kundi hilo la watu wanaoamini hivyo lakini pia wapo baadhi ya watu huamini ya kwamba mapenzi hayana faida yeyote ile.
Kundi hili la watu hao hujikuta wakitoka kwenye mahusiano, na sababu zinazopelepekea wao waamini hivyo mara nyingi huwa zinatokana na maumivu ya kutendwa na mtu ambaye alikuwa anamuamini na leo hii hayupo na mtu huyo tena kwenye mahusiano.
Tumekusogezea faida za kuwa single katika ulimwengu huu.
1. Mtu anapokuwa single anakuwa na uhuru wa muda wa kufanya mambo yako binafsi pasipo kupelekeshwa na mtu yeyote yule. Uhuru huu wa muda ni ule wa kufanya mambo yake na ya kijamii pia.
2. Mtu ambaye yupo single unakuwa na uhuru pia wa kufanya kile inachokitaka/ anachokipenda. Unapokuwa kwenye mahusiano kunakosekana uhuru wa kufanya vitu uvipendavyo hii ni kwa sababu unaweza ukawa unapenda kufanya jambo fulani ila kwa kuwa upo kwenye mahusiano ya kimapenzi huyo mpenzi wako akakuzuia kufanya jambo hilo kwa kuwa jambo hilo halimpendezi.
3. Unapikuwa single unakuwa hauna hisia mpelekesho, hisia mpelekesho ni zile hisia za kimapenzi ambazo zinakufanya ifikiri sana kuhusu mambo yanayohusu mapenzi, kwa mfano hivi hujawahi ona mtu anakurupuka usiku wa manane anampigia simu mpenziwe? bila shaka umewahi kuona, hii ni tabia inayokwenda sambamba na kitu kinachoitwa wivu.
4.Ukiwa singo unajiondolea shida ya kuwa na bajeti zisizo na maana,Kwa watu ambao bado wanatafuta maisha hii ni point kubwa sana kwao,kama unataka kufanikiwa kimapenzi haupaswi kufanya mapenzi yawe sehemu kubwa kwako kwani yatakupotezea muda na fedha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment