Thursday, June 13, 2019

JINSI YA KUZUNGUMZA NA MPENZI WAKO

Mnakubaliana nam kuwa kupenda mtu ni tofauti na kuishi kwa upendo. Kumpenda mtu ni rahisi lakini kwa kuishi huo upendo, yaweza kuwa ngumu kidogo. Ian Isherwood anasema kuwa kurudiarudia huu mshororo wenye maneno matatu tu, “I Love You” Mara kwa mara haitoshi kuweka mapenzi ya uhusiano wenu kunoga zaidi milele. Kuna Sentensi sita muhimu sana ukimwambia mpenzio mara kwa mara napenzi yenu yafikia upeo.
Kila mtu ana njia yake ya kumwonyesha mpenzi wake kuwa anampenda na kumjali. Haijalishi ni maneno yepi hutumia. La maana ni kwamba uhusiano wake na mpenziwe unadumu kwa raha tele.
Ukitumia maneno mazuri kwa mpenzi wako unampa furaha na kumwonyesha kuwa yeye ndiye mtu wa kipekee kwako duniani. Kama unaye mpenzi, anza kutumia , maneno haya sita na uhusiano wako utakuwa wenye raha;
1.  Nimebahatika kuwa nawe
Kumwelezea mpenzio vile unajisikia kubahatika kuwa naye katika maisha yako ina uzito zaidi kuliko ” Love You”. Wakati unampenda mtu sana unajiona duni kwamba hata kuona amekufanyia fadhila ({Favour) kuwa nawe. Yaani ni kama huna cha kumrudishia kama shukrani kwa upendo wake kwako. Ukisema haya wamfanya kujiskia amependwa na kwamba unafurahia anayokufanyia.
2. Pole/ Samahani
Kusema Pole baada ya kukoseana au majibizano madogo huongeza mapenzi katika ndoa yenu. Kusema “pole” haitamaanishe eti wewe ni hafifu sana kumliko mwenzio. Kila ndoa huwa na majibizano, wivu na kutoelewana. Lakini baada ya hayo yote, sema “pole” na kwa ukweli yatapoa!
3. Nimekusamehe 
Ni vigumu kwa mtu kuomba msamaha lakini ni vigumu zaidi kusamehe mtu. Msamaha ni jambo muhimu sana katika uhusiano.  Ni ngumu sana kuifanya mara kwa mara lakini ndiyo huongoza na kupeana mwelekeo wa ndoa. Haina haja kushikilia mabaya ili kuharibu ndoa yako. Msamehe tu!
4. Nipo hapa kwa ajili yako 
Wakati mwenzako anapitia magumu, hakuna maneno yanayompa nguvu kuliko ” Nipo hapa kwa ajili yako” kutoka kwa ampendaye. Maneno haya humhakikishia mwenzio kuwa una yeye katika hali zote za kimaisha
5. Nakuamini 
Bila kuaminiana ndoa haiwezi dumu. Ndoa hupata majaribu hata ikiwa ya miaka hamsini! Lakini la muhimu sana ili kudumisha mapenzi katika ndoa ni uaminifu. Ukimwambia mwenzako unamuamini, basi umeondoa hisia za mbaya kumhusu kama wivu ambao ni hatari sana kwa ndoa.
6. Nijitolea kwako kikamilifu 
Kujitolea kwa hakika kwa mpenzio huonyesha kuwa ulimchagua yeye pekee, kawa mwaminifu na kampeda kwa dhati. Kila mtu hutaka kuhakikishiwa kuwa ni yeye tu katika uhusiano. Usione ni kawaida kuwa na mpenzio.  Kama kukushawishi mshiriki mapenzi ama kujinufaisha kifedha. Usidanganyike! angalia pia matendo yao kama yanaambatana na maneno yao.

No comments:

Post a Comment