Friday, June 28, 2019

MANENO AMBAYO MWANAUME HUPENDA KUAMBIWA


Kwenye suala la mahusiano ya kimapenzi kuna mambo mengi ambayo yanaweza kuimarisha penzi na kulipa mizizi imara ili kuweza kudumu zaidi kama wapenzi watakuwa na nia moja. Leo tuangalie Mambo 5 Ambayo Mwanaume Hupenda Kusikia Toka Kwa Mpenzi Wake.
1. Kukosolewa – “I think you are wrong”
Wanaume wanaweza kujikweza sana lakini daima hawachukii kurekebishwa. Wanachojali zaidi ni jinsi gani au njia gani imetumika kuwarekebisha. Mwanaume akikosea, anataka mpenzi wake amkosea lakini kwa mapenzi, sio kwa mikwaruzano au dharau au mbele ya kadamnasi. Mrekebishe au mkemee faragha, toa maoni yako na wala usimlazimishe, itamfanya aone unajali na unataka kumjenga.
2. Kujali – “How was your day?”
Wanawake wengi hutaka wao tu ndio waulizwe kuhusu jinsi siku zao zilivyoenda kila siku, wanasahau kabisa hata wanaume nao walikua kwenye mihangaiko. Mzoeshe kumuuliza mpenzi wako siku yake ilikuwaje? utaona hata nuru ya mapenzi yenu itang’aa na mtakua marafiki, japo mwanzoni atakua hakuambii kila kitu lakini baada ya muda atazoea. Kila mtu anataka wa kumsikiliza, mtu atakayezungumza nae chochote kilichotokea ndani ya siku yake, na pengine kukuuliza ushauri.
3. Ucha Mungu – “Can we pray?”
Mwanaume, anayesali au kutosali, lazima huwa ana imani kwamba Mungu yupo. Mwanamke mcha Mungu siku zote huwa ni wazo la kila mwanaume endapo ana mpango wa kuoa. Mwanaume huwa na amani kwa kiasi fulani akiongozwa na mwanamke wake kwa upande huo wa sala.
4. Msamaha – “I forgive you”
Vikombe kwenye sahani haviko na uwiano sawa kuna muda vinaweza vikagongana,ikiwa umemuudhi mumeo jaribu kumuomba msamaha hii itasaidia sana
5.Kutiwa moyo—"bby take easy"
Wanaume wengi wanakutana na changamoto nyingi katika harakati zao utafutaji kila siku hivyo ni vyema mwanamke uwe bega kwa bega kumpa moyo

No comments:

Post a Comment