Saturday, June 29, 2019

NJIA ZA KUFANYA ILI MWANAUME AKUOE


Kumfanya mwanaume aweze kuwa na majukumu ya kimaisha ni vigumu, lakini hizi mbinu ambazo tuko nazo za kumfanya mwanaume akuoe zitahakikisha umesimama na yeye madhabahuni haraka sana.
Hivi wewe umekuwa katika mahusiano na mwanaume kwa muda mrefu mpaka unaanza kushuku iwapo huyu mwanaume yuko serious na wewe ama anakuchezea tu? Na umekuwa kila siku ukimwomba Mola akusaidie angalau amfanye huyu mwanaume ulie naye atoe ishara za kuwa atakuoa mbeleni.
Well, sote tunajua kuwa ndoto ya kila mwanamke ni kuwa siku moja katika maisha yake atakuja kuolewa kwa harusi…so sisi hapa tunataka kukupa maujanja ya kumfanya huyo mwanaume atake kukuoa haraka sana.
Zama nasi.
1 Kuwa girlfriend kamili. Hivi wewe na mwanaume huyu mumekuwa na maisha ya fanaka. Nyote wawili mumeinjoy maisha ya furaha, mumezama katika mapenzi, na unaona kwamba una uwezo wa kumwambia kila kitu ambacho unakifikiria. Lakini hebu ngoja kidogo na ufikirie mambo ambayo unaweza kufanya zaidi ya hayo.
Mfanye ajihisi kuwa anakubalika, yuko salama na special, haya ndio mambo ambayo anahitaji zaidi. Bila shaka utakuwa unamjua zaidi ya mtu yeyote yule. Kile ambacho anapenda na kuchukia, na mambo ambayo yatamfanya akuone kuwa wewe unapendeza zaidi ya kitu chochote kile.
Hakikisha unafanya kila kitu ambacho mwanamke kamili anaweza kufanya. Mwonyeshe kila kitu ambacho anahitaki, na bila shaka atakuona wewe umejitweka jukumu la kuhakikisha kuwa wewe uko hapo kwa ajili yake.
2 Mtunze. Kama mwanaume anahisi kuwa hawezi kuishi bila wewe, basi bila shaka atahakikisha ametia kufuli jambo hilo.
Hakikisha kuwa unamtunza na unamfanya akutegemee kwa mambo madogo madogo, hata kama ni jambo rahisi lile la kushughulikia nguo zake ama kumpa sapoti wakati anapohitaji. Wewe kuwa ubavuni mwake kutafanya mabadiliko ya haraka sana, na hatoweza kustahimili kuishi bila wewe.
3 Kuwa shabiki wake mkuu. Jeuka shabiki mkuu wa mwanaume wako. Kitu chochote kile ambacho ayaamua kufanya, hata kama ni jambo la utani ama la kuchekesha wewe mpe sapoti kwa kumshabikia atimize azma yake.
Ile siku ambayo atakuja kugundua kuwa mafanikio yake katika azma yake yamechangiwa na wewe basi atakuweka karibu yake. Atakuona kuwa wewe umekuwa karibu yake bila hata kupoteza imani katika azma yake. Well utakuwa umetoboa.
4 Mtreat. Wakati mwingine wanaume huchoka kwa kuwa wao ndio kila wakati huwatoa wanawake out na deti. Msaprize siku moja kwa kumtoa out siku moja, na kuhakikisha unafanya mambo ambayo anapenda kufanya.
Tumpeleka sehemu romantik, kumtoa katika dinner na kumuonyesha jinsi romance inavyokuwa kutamfanya achangamke na labda anaweza ingiwa na jazma ya kukutamkia lile neno ambalo umekuwa ukilingojea kutoka kwake kwa miaka.
5 Kuwa mkweli kwa kile unachotaka. Wanaume wengi si wajuzi wa kusoma akili ya mtu. Wakati mwingine unaweza kuwa katika mahusiano na mwanaume kwa miaka mingi na ukashangaa ni kwa nini mwanaume kama huyu hajakuposa. Kuna uhakika mkuu ni kuwa wazo kama hilo bado halijamlenga kwa kichwa chake.
Kama umekuwa na maongezi ya ukweli na mwanaume wako, na ukaweka wazi kuwa unampenda, na ukaeleza vile ambavyo unaona mahusiano yenu yatakuwa miaka inayokuja, basi anaweza kuingiwa na hali ya kutaka kuchukua hatua ya mbele kuhusiana na unavyosema. Hata kama hana uhakika na ndoa, atleast utakuwa umeliweka wazo hili katika kichwa chake.
6 Usiwe comfortable sanaa. Kuwa comfortable sana katika mahusiano ni hatari sana. Haswa iwapo kama unataka mwanaume wako achukue hatua ya mbele. Ni rahisi kujisahau katika hali ulioko wakati huo na mwishowe kuwa mvivu. La kufanya ni kuhakikisha kuwa unatafuta maisha yako wewe mwenyewe, interests zako na marafiki wa kwako.
Hakuna kitu kizuri zaidi kama mwanamke ambaye ana uwezo wa kujitegemea mwenyewe. Mfanye akuone kuwa wewe una mambo yako ambayo unafanya, na kuwa una maisha yako ya nje kando na kuwa katika mahusiano. Soon ataanza kuona jinsi ilivyo rahisi kwako kuenda zako, na hivyo atahakikisha ya kuwa jambo kama hilo halitokezei.
7 Usimuogopeshe. Usimuogopeshe mwanaume ili akupose kwa kuwa hilo si jambo la kufuata. Inakubalika kuongea maswala ya ndoa, na kueleza msimamo wako. Lakini iwapo utakuwa kila wakati unamtia presha, kila wakati unagusia swala la ndoa, ama kuanza kutokwa na machozi kila upitapo mbele ya duka la harusi basi utafanya ile dhana ya kwake kukuoa kufifia haraka sana kwani atakuogopa.
8 Mwonyeshe kuwa wewe ni wife material anayemwota. Ukimwona mwanaume ameamua kuwa wewe ndie aliyekuchagua basi tayari alikuwa alikuweka kwa ndoto zake awali.
Kama unamtaka aweke pete kwa kidole chako, basi mwonyeshe kuwa wewe utakuwa mke mwema. Kuwa mtiifu, mwaminifu, mpole, mvumilivu, na mpendezi. Muda si mrefu ataona kuwa hakuna mwanamke yeyote ambaye anaweza kuzishinda tabia ambazo uko nazo.
9 Rudi nyuma. Kama imepita muda mrefu na umeshajaribu mbinu zote tulizozitaja hapo juu, basi jambo la mwisho ambalo unaweza kufanya ni kurudi nyuma kiasi. Kumpatia mwanaume wako nafasi ya kupumua si jambo baya, Si lazima ufanye mambo mazito ya kuleta atenshen ya bure. Kwa kupoa kiasi, anaweza kuhisi kutokuwepi kwako na kugundua kuwa maisha yatakuwa hayana maana kama hautakuwa na yeye.
Atagundua kuwa maisha yake ni mahumu bila wewe na hapo hapo atakutaka uwe na wewe zaidi kuliko awali.
10 Mtamkie. Wakati mwingine kufunguka ni jambo zuri. Kama umechoka kungojea, mbona usichukue hatua mikononi mwako na kumwambia akuoe mwenyewe?

No comments:

Post a Comment